SERENGETI BOYS WATWAA UBINGWA WA CECAFA CHALLENGE U17 BURUNDI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, April 29, 2018

SERENGETI BOYS WATWAA UBINGWA WA CECAFA CHALLENGE U17 BURUNDI

TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge U-17 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia jioni ya leo Uwanja wa Ngozi mjini Bujumbura, Burundi.
Ushindi huo umetokana na mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66 katika mchezo ambao Serengeti Boys ilionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafurahisha mashabiki.
Image result for serengeti boys

Ikumbukwe Somalia imefika hatua hii baada ya kuwatoa Uganda, wakati Tanzania iliwatoa Kenya katika mechi za Nusu Fainali. 
Katika fainali hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad alikuwepo na kukabidhi Kombe kwa mabingwa, ambao msafara wao uliongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.

No comments:

Post a Comment