MICHEZO Serengeti Boys watinga fainali Burundi - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 25, 2018

MICHEZO Serengeti Boys watinga fainali Burundi

Image result for serengeti boys
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) imekata tiketi ya kucheza hatua ya fainali ya michuano ya Afrika mashariki na kati inayoendelea mjini Bujumbura nchini Burundi.
Serengeti Boys inayonolewa na kocha Oscar Milambo imefanikiwa kupiga hatua hadi kwenye mchezo wa fainali baada ya kuibanjua Kenya mabao mawili kwa moja katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa leo jioni, uwanja wa Muyinga.
Mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Jaffari Juma dakika ya 21 na Calvin Paul dakika ya 62.
Mchezo wa fainali utachezwa Uwanja wa Ngozi April 29 kati ya Serengeti Boys dhidi ya Somalia ambao waliifunga Uganda bao moja kwa sifuri katika mchezo uliotangulia mapema hii leo.
Mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu utazikutanisha Uganda na Burundi April 28, Uwanja wa Ngozi.

No comments:

Post a Comment