MCHEZAJI HUYU KUKOSA KARIAKOO DERBY - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 25, 2018

MCHEZAJI HUYU KUKOSA KARIAKOO DERBY

Image result for niyonzima

Unaweza kusema huu ni mwaka wa shida kwa Haruna Niyonzima.

Niyonzima ambaye tokea amejiunga na Simba amekuwa akihaha nje ya uwanja kwa kuwa nje ya uwanja kutokana na kuandamwa na majeraha.

Lakini leo amepata msimu wa kufiwa na dada yake ambaye imeelezwa anaitwa Hawa Sumaya Twizemana.

Niyonzima anatarajia kuondoka kurejea kwao Kigali ili kuhudhuria mazishi ya dada yake huyo.

Maana yake, sasa ataikosa mechi dhidi ya watani wao Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Niyonzima hakuwa na uhakika wa kuanza, lakini angeweza kukaa benchi Jumapili kwa kuwa tayari alisharejea uwanjani.

No comments:

Post a Comment