1.Suarez huyu ni staa wa soka wa timu ya taifa ya Uruguay ambaye kwa sasa anaichezeaFC Barcelona ya Hispania, akiwa na umri wa miaka 12 Suarez alikuwa akicheza mpira pekupeku kutokana na familia yake kushindwa kumudu kumnunulia viatu, Suarez amezaliwa katika familia ya watoto saba yeye akiwa wanne na akiwa na umri wa miaka 9 baba na mama yake walitengana, Suarez wakiwaMontevideo aliendeleza kipaji chake kwa kucheza mtaani lakini pia alikuwa akifanya kazi za kufagia mtaani.
2- Luka Modric huyu ni moja kati ya viungo bora wa timu ya taifa ya Croatia na club ya Real Madrid ya Hispania lakini akiwa na miaka 6 mwaka 1991 vita vya Croatia ambavyo vilimpelekea baba yake kuungana na jeshi vilimfanya yeye na familia yake kwenda kuishiKolovare katika kambi ya wakimbizi kwa miaka saba.
3- Carlos Tevez amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama West Ham na Man United na sasa yupo kwao Argentinaanaichezea Bocca Junior, Tevezamekulia Fuerte Apache nchini Argentina moja kati ya sehemu hatari zaidi na wanaishi watu masikini na kuna matukio mengi ya kiharifu na uuzwaji wa dawa za kulevya, kuharibika kwa meno yake kunatokana na matukio ya ugomvi aliyokuwa anapitia katika mtaa aliokulia.
4- Cristian Ronaldo ni moja kati ya wanamichezo matajiri katika hii dunia kwa sasa na mara yake ya kwanza anapanda ndege ilikuwa ni wakati anakwenda kusaini Man United, kabla ya hapo Ronaldo amekulia katika familia ya kimasikini Ureno na ilifika wakati akawa analala chumba kimoja na dada zake kutokana na ugumu wa maisha licha ya kuwa umri ulikuwa unataka awe na chumba chake.
5- Dani Alves amecheza FC Barcelona,Juventus na sasa PSG ya Ufaransa, Alveswakati akiwa mdogo alikuwa akilazimika kuamka saa 10 alfajiri ili kwenda na baba yake kumsaidia katika shughuli zake za kila siku na alikuwa akilala katika kitanda kibaya, pamoja na ugumu wa maisha hayo aliyoyapitia Alvesamewahi kukiri kuwa alikuwa ameridhika nayo.
6- Zlatan Ibrahimovic ambaye ameichezea Man United na sasa LA Galaxy ya Marekani alizaliwa wilaya ya Rosengard katika mji waMalmo nchini Sweden, Zlatan amekuwa akiwa na sifa mbaya na ametokea katika familia ya kimasikini, baiskeli aliyokuwa anaitumia kwenda nayo mazoezini ilikuwa ya wizi.
7- Neymar JR ambaye kwa sasa anatazamiwa kuja kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka ya baadae, amelelewa katika nyumba ya babu yake ambapo alikuwa analelewa katika chumba duni sana na alikuwa akishea chumba hicho yeye, wazazi wake na dada yake.
8- Alex Sanchez kwa kiasi kikubwa maisha yake ya utotoni amelelewa bila uwepo wa baba yake na alikuwa akifanya kazi za kuosha magari ili aweze kuisaidia familia yake nchiniChile, Sanchez anamini kama sio mpira basi asingekuwa chochote katika hii dunia.
9- Frank Riberry amekulia ghetto Kaskazini mwa nchi ya Ufaransa na aliepuka kuishi maisha ya bila kuwa na kazi kwa kuanza kufuata ndoto zake za kucheza mpira kitu ambacho kimemkomboa katika maisha yake na kufanya dunia nzima kumjua kwa uwezo wa
No comments:
Post a Comment