Kocha wa Yanga ahitajika Zambia, sasa kuvunja mkataba na wababe hao - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, April 10, 2018

Kocha wa Yanga ahitajika Zambia, sasa kuvunja mkataba na wababe hao

Image result for lwandamina
Mabingwa wa soka nchini Zambia, Zesco United wanatarajia kumthibitisha wiki hii kocha George ‘Chicken’ Lwandamina kuwa mwalimu mkuu wa timu hiyo.
Taarifa hiyo imeandikwa na tovuti ya Zambianobserver, ambapo imeelezwa kuwa Lwandamina tayari amekwisha kusaini mkataba wa awali wa kuanza kuifundisha timu hiyo kuanzia mwezi ujao.
“ Labda kama Lwandamina na Yanga watafikia makubaliano, atajiunga nasi mwezi ujao “ amesema mmoja wa viongozi wa Zesco United.
Lwandamina ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya Yanga mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu.
Aidha, Lwandamina anatajwa kutakiwa kuchukua nafasi ya kocha Tenant Chembo aliye jihuzulu kuifundisha timu hiyo hivi karibuni na kujiunga na Buildcon inayo shiriki ligi kuu nchini Zambia.
Hata hivyo, Mpaka sasa klabu ya Yanga haijazungumza chochote kuhusu mkataba wa kocha huyo anayetarajia kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya nchini Ethiopia.

No comments:

Post a Comment