Wanariadha wa Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda wanatarajiwa kupambana vikali Jumatatu wiki hii katika fainali ya mbio za mita elfu kumi kwenye michezo ya Jumuiya ya Madolamjini Gold Goast.
Kuna kivumbi hapo kwani Wakenya wana hasira mno ya kulipiza kisasi kutokana na ushindi wa Joshua Cheptegei wa Uganda Jumapili mbio za mita elfu tano.
Kuna kivumbi hapo kwani Wakenya wana hasira mno ya kulipiza kisasi kutokana na ushindi wa Joshua Cheptegei wa Uganda Jumapili mbio za mita elfu tano.
Ni ushindi ambao haujawafurahisha hasa kuangushwa na mkimbiaji wa Uganda ambao kwa miaka mingi wamekua hawababaishi wakimbiaji wa Kenya.
Wakimbiaji wa Kenya wanaotegemewa sana kufanya vyema ni Sandrafelis Chebet ambaye alizaliwa Kericho Januari tarehe 20 1998 ,Stacy Ndiwa na Beatrice Mutai..
Wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mkimbiaji wa Rwanda Salome Nyirarukundo ambaye amefanya mazoezi nao eneo la bunde la ufa..
Kutoka Tanzania kuna Failuna Matanga na waakilishi wa Uganda Mercyline Chelangat, Juliet Chekwel na Stella Chesang.
No comments:
Post a Comment