BENO KAKOLANYA ANAHUSISHWA KUNYATIWA NA KLABU HII NCHINI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, April 17, 2018

BENO KAKOLANYA ANAHUSISHWA KUNYATIWA NA KLABU HII NCHINI

Image result for Beno Kakolanya
Kipa wa zamani wa Tanzania Prisons na Young Africans, Beno Kakolanya, inaelezwa kuwa anawindwa na timu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

Singida United inatajwa kama timu mojawapo inayowania saini ya kipa huyo ambaye amekosa namba kwenye kikosi cha Yanga.

Beno alijiunga na Yanga akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya lakini alishindwa kudumu katika kikosi cha kwanza kufuatia uwepo wa aliyekuwa mlinda mlango wa timu hiyo, Deogratius Munish 'Dida' na sasa Youthe Rostand.

Matajiri hao wa Singida wanahusishwa na wachezaji wawili sasa kutoka Yanga ikiwemo winga Geoffrey Mwashiuya aliyesajiliwa kutoka Kimondo FC.

Tetesi hizi zimeanza kuja kutokana na wachezaji hawa wawili kutokuwa sehemu ya kikosi cha kwanza haswa Kakolanya ambaye hajacheza kwa muda mrefu langoni.

No comments:

Post a Comment