24 Lipuli Fc waifuata Mbao fc - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 2, 2018

24 Lipuli Fc waifuata Mbao fc


Nyota 24 wa klabu ya Lipuli wameondoka  alfajiri ya leo kuelekea Kanda ya ziwa ambako watakwenda kucheza michezo miwili ya ligi kuu Tanzania bara ambao mchezo wa awali utakuwa dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa april 6 na Mwadui Fc.

Katika kuhakilisha timu hiyo inafanya vyema katika michezo hiyo timu hiyo imekiwa ikifanya mazoezi mara mbili kila siku ambapo imekuwa ikifanya mazoezi Asubuhi na Jioni.

Aidha msemaji wa klabu hiyo, Clement Sanga amesema kikosi hicho kipo katika hali nzuri na wachezaji wana ali na molali kwa kila mmoja huku akisema hakuna majeruhi hata mmoja.

Hata hivyo amewataka wapenzi, wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo  kuendelea kuichangia kifedha ili kuhakikisha wanaiwezesha timu hiyo kifedha ili kuona kama inaweza kufanya vyema katika michezo iliyosalia.

"Ila tu naendelea kuwasisitiza wanachama, Wapenzi na Mashabiki wetu kuendelea kutuchangia kwani mpaka sasa hali ya timu kifedha sio nzuri sana , kwa hiyo tunawaomba sana kwa namna moja ama nyingine
Muweze kushiriki katika kugakikisha ya kwamba timu inakuwa katika nafasi nzuri kifedha". Amesema Sanga.

Kuhusu orodha ya wacgezaji Sanga amesema itawekwa hadharani wakati wowote kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment