Thomas Ulimwengu habebwi Taifa stars ya Mayanga - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, March 18, 2018

Thomas Ulimwengu habebwi Taifa stars ya Mayanga


Moja kati ya taarifa zilizokuwa zimewashitua wengi ni baada ya jina la Thomas Ulimwengu kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa ajili ya michezo ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DRC Congolakini wakihoji Ulimwengu ameitwa mbona hana timu kabla ya kugundulika kuwa anacheza FK Sloboda ya Bosnia.
Ulimwengu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha lake la goti na kuachana na timu yake ya AFC Eskilstuna ya Sweden, wiki iliyopita aliripotiwa kuwa amejiunga na club ya FC Sloboda ya Bosnia lakini hakuwa amepata nafasi ya kuichezea kwa sababu ya kukosa vibali vya kufanyia kazi na kuishi.

No comments:

Post a Comment