NYOTA EVERTON AMPA ULAJI KICHUYA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, March 29, 2018

NYOTA EVERTON AMPA ULAJI KICHUYA

Image result for bolasie
Mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie ambaye alikuja nchini Tanzania na kikosi cha DR Congo kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania juzi, amevutiwa na kiwango kilichoonyeshwa na winga wa Simba Shiza Kichuya.

Katika mchezo huo Shiza Kichuya alifanikiwa kufunga goli la pili, mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam Tanzania ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Nyota huyo muhimu katika kikosi cha Simba pia alitengeneza goli la kwanza lililofungwa na nahodha wa Stars Mbwana Ally Samatta.
Image result for kichuya
Yannick Bolasie amesema Kichuya ana kiwango cha kusakata kabumbu Barani Ulaya na akasema kama atapata wakala mzuri hatachelewa kupata timu.

Inasemekana kuwa mkataba wa nyota huyo  unafikia mwishoni mwa msimu huu, licha ya uongozi wa Simba kufanya juhudi kubwa za kutaka kumuongezea mkataba mapema, mwenyewe amegoma kusaini mkataba mpya hadi mwishoni mwa msimu. 

No comments:

Post a Comment