BUYERN MUNICH KUMTOA TUCHER DORTIMUND - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, March 27, 2018

BUYERN MUNICH KUMTOA TUCHER DORTIMUND

Image result for thomas Tuchel
Bayern Munich ndio chaguo la kwanza la kocha Thomas Tuchel kama akirejea madarakani tena na Mjerumani huyo hana mpango wa kuchukua mikoba ya Arsene Wenger kama aking'atuka Arsenal.

Vinara wa Bundesliga wameanza mchakato wa kutafuta mrithi wa kocha Jupp Heynckes ambaye ataachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.

Tuchel aliachia ngazi katika klabu ya Dortmund mwezi Mei mwaka jana na amekuwa akisubiri fursa sahihi kuwasili.

Taarifa kutoka Ujerumani juzi zilisema kwamba Tuchel ameikataa Bayern na anaitaka Arsenal lakini leo Sky sports imearifu kwamba Mjerumani huyo anataka kuinoa Bavaria.

Na mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote baina ya wawakilishi wa Tuchel na Arsenal.

Pia imearifiwa kwamba endapo ataikosa Bayern Munich basi yupo tayari kufanya kazi Uingereza , lakini atakuwa tayari kufundisha klabu ambayo ina hadhi ya Ukubwa wa Ulaya  na ile inayocheza mashindano ya Ulaya. 

No comments:

Post a Comment