Droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanyika Desemba 1 Urusi - ALEX MWENDATZ

Breaking

Thursday, November 16, 2017

Droo ya Kombe la Dunia 2018 kufanyika Desemba 1 Urusi

Baada ya mataifa 32 kufanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Urusi, droo ya kupanga makundi ya timu hizo itafanyika Ijumaa ya Desemba 1 mjini Moscow.
Kuelekea zoezi hilo baadhi ya Timu ambazo zimepangwa chungu kimoja ni chungu cha kwanza ambacho kina timu mwenyeji Urusi, Ujerumani, Brazil, Ureno, Ajentina, Ubelgiji, Poland na Ufaransa.
Afrika inawakilishwa na Misri, Nigeria, Morocco, Tunisia na Senegal.
Na kuelekea fainali hizo FIFA wamesema mpaka sasa kuna maombi milioni 3.5 ya tiketi na walioomba wengi wao ni wenyeji Urusi.

Vyungu vimepangwa vipi?

Vyungu Kombe la Dunia
Chungu 1Chungu 2Chungu 3Chungu 4
Urusi (wenyeji)Uhispania (8)Denmark (19)Serbia (38)
Ujerumani (1)Peru (10)Iceland (21)Nigeria (41)
Brazil (2)Uswizi (11)Costa Rica (22)Australia (43)
Ureno (3)England (12)Sweden (25)Japan (44)
Argentina (4)Colombia (13)Tunisia (28)Morocco (48)
Ubelgiji (5)Mexico (16)Misri (30)Panama (49)
Poland (6)Uruguay (17)Senegal (32)Korea Kusini (62)
Ufaransa (7)Croatia (18)Iran (34)Saudi Arabia (63)
Kombe la Dunia

No comments:

Post a Comment