NYOTA wa Bayern Munich, Renato Sanches anakaribia kuwa mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo ikiwa atacheza mechi moja zaidi kabla ya mwishoni mwa msimu.
Kiungo wa Ureno alijiunga na The Bavarian msimu uliopita kwa dau la Pauni Milioni 30, lakini linaweza kupanda hadi kufika Pauni Milioni 67.
Wakati rekodi yao ya sasa ya kusajili mchezaji wa bei kubwa ikiwa ni Pauni Milioni 33 walizotoa kumsajili Javi Martinez, inaonekana unasubiriwa wakati tu kabla ya Sanches kupiku rekodi hiyo.
Na hiyo ni endapo mwishoni mwa wiki ijayo atapangwa wakati Bayern Munich watakapomenyana na Darmstadt 98.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la Ujerumani mchezo mmoja zaidi utaifanya Benfica ingize Pauni Milioni 4 iwapo atafikisha mechi 25 msimu huu.
Baada ya kutokea kwenye benchi dhidi ya Wolfsburg, sasa amefikisha mechi 24.
Sanches, ambaye hakutarajiwa kucheza kwa kiasi hiki wakati anahamia Allianz Arena, ameanzishwa katika mechi tano tu za Bundesliga, lakini amekuwa akitokea benchi mara 11. Pia amecheza mechi mbili za Kombe ka Ujerumani, maarufu kama DFB-Pokal na sita za Ligi ya Mabingwa Uklaya.
Mchezo mmoja zaidi utatosha kumfanya ampiku Martinez, aliyejiunga na timu hiyo kutoka Athletic Bilbao mwaka 2012.
Akiwa ametoka kujihakikishia taji la Bundesliga kwa ushindi wa 6-0 dhidi ya Wolfsburg mwishoni mwa wiki iliyopita, Carlo Ancelotti anatarajiwa kubadilisha kikosi chake katika mechi zijazo dhidi ya Darmstadt, RB Leipzig na Freiburg.
No comments:
Post a Comment