Mbeya City washindwa kuibeba Simba, Mbao na Ndanda hali tete - ALEX MWENDATZ

Breaking

Saturday, May 13, 2017

Mbeya City washindwa kuibeba Simba, Mbao na Ndanda hali tete


Mbeya City washindwa kuibeba Simba, Mbao na Ndanda hali tete



Matumaini ya Simba kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania yamezidi kufifia baada ya hii wapinzani wao wakubwa, Yanga kujifagilia njia kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.

Yanga ilipata ushindi huo kupitia kwa mabao ya Simon Msuva aliyefunga kwa kichwa mnamo dakika ya 8 tu ya kipindi cha kwanza na Obrey Chirwa akafunga bao la pili na la ushindi.
Haruna Shamte aliiswazaishia Mbeya City kwa shuti la ndani ya kumi na nane kabla ya bao la Chirwa kufifisha matumaini ya Simba.

Kwa matokeo haya Simba itaomba Yanga idondoshe idondoshe iangushe angalau pointi nne kuweza kubeba ubingwa.

Kwa upande mwingine vita ya kuepuka kushuka daraja imezidi kupamba moto baada ya Majimaji kuibuka na ushindi muhimu dhidi ya JKT Ruvu wa bao 1-0 na kujinasua katika timu tatu za mkiani.
Matokeo mengine yalishuhudia Ndanda ikizamishwa na Prisons kwa mabao 2-1 na kujiweka katika nafasi mbaya zaidi ya kuteremka.

Mjini Bukoba, Mbao waliruhusu bao la dakika ya mwisho na kujikuta wakipigwa mabao 2-1 na Kagera Sugar matokeo ambayo yamewashusha hadi nafasi ya nne kutoka mkiani na hivyo kujitaji ushindi dhidi ya Yanga kuwa uhakika wa kubaki Ligi Kuu msimu ujao.
Matokeo kamili ya leo:
Yanga 2-1 Mbeya City
Mtibwa Sugar 4-2 Mwadui
Kagera Sugar 2-1 Mbao
Prisons 2-1 Ndanda
JKT Ruvu 0-1 Majimaji

No comments:

Post a Comment