OKWI AIPIGIA MAHESABU SIMBA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, May 29, 2017

OKWI AIPIGIA MAHESABU SIMBA

Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi aliyemaliza mkataba wake na klabu ya SC Villa ameendelea kuonesha kiwango kizuri.
Siku ya Jumapili, Okwi alifunga mabao mawili katika mechi ya kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kwa wachezaji wa ndani dhidi ya kombaini ya jimbo la Kitara.
Okwi na wachezaji wenzake wakishangilia ( Picha FUFA)
Uganda Cranes ilishinda mabao 3-0 katika pambano hilo la maandalizi ya mechi ya CHAN dhidi ya Somalia.


Okwi amemamaliza mkataba wake na SC Villa huku akiifungia mabao 10 katika mechi 13 za Ligi alizocheza baada ya kusajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili nchini humo.

No comments:

Post a Comment