Kwa takwimu hizi Arsenal walistahili kipigo kutoka kwa Palace - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, April 11, 2017

Kwa takwimu hizi Arsenal walistahili kipigo kutoka kwa Palace

Arsene Wenger wazungu wanamuita “White Mugabe” wakimaanisha ni mzungu mwenye tabia za Robert Mugabe. Ni miaka 88 sasa imepita tangu Arsenal wafungwe magoli matatu tatu katika michezo minne mfululizo ya ugenini na mechi dhidi ya Palace Wenger amevunja rekodi hiyo, kwa takwimu zifuatazo zinaonesha ni lazima Arsenal walistahili kipigo kutoka kwa Palace.

1.Arsenal hawakupiga hata shuti moja golini kwa Crystal Palace kipindi cha pili. Huwezi kupata ushindi huku washambuliaji wako hawaoneshi utashindaje, timu nzima ya Arsenal wakiongozwa na mshambuliaji wao Alexis Sanchez hawakupiga hata shuti moja golini mwa Crystal Palace katika kupindi cha pili.

2.Shkordan Mustafi hakufanikiwa tackle hata moja katika 6 alizofanya. Kwa vijana wa huku tunaita “katoa boko”, kwani Mustafi alikuwa akipambana kufanya ukabaji lakini takwimu zinaonesha katika tackle zake 6 alizojaribu kufanya, alizipoteza zote.

3.Mamadou Sakho ametengeneza nafasi nyingi kuliko Ozil na Sanchez. Katika mchezo huo Mesut Ozil hakutengeneza hata nafasi moja huku Sanchez akitengeneza moja, wakati beki wa Crystal Palace Mamadou Sakho alitengeneza nafasi mbili.

4.Arsenal wameruhusu magoli matatu kwa kila mchezo wa ugenini katika mechi 3 kabla ya kukutana na Crystal Palace. Walifungwa 3 na West Brom ugenini, wakafungwa 3 na Liverpool ugenini, wakafungwa 3 na Chelsea ugenini hii iliwapa imani Palace nao kuwafunga 3, hii ikiwa rekodi mbaya kwao tangu mwaka 1929.

5.Arsenal wamefungwa magoli mengi kuliko timu iliyoko nafasi ya 19. Arsenal walioko nafasi ya 6 hadi sasa wamefungwa magoli 39 huku Middlesbrough walioko nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi hadi sasa wamefungwa mabao 37.

No comments:

Post a Comment