Kimwana wa Cristiano Ronaldo imemlazimu kuachana na kazi yake ambapo alikuwa ni meneja mauzo katika kampuni ya Prada.
Georgina Rodriguez ambaye alikuwa anapokea kiasi kinachokaribia
paundi £1,370 kwa mwezi kwa kamisheni pekee kila mwezi ameamua kuondoka
kwenye kiti chake hizo kutokana na rundo la waandishi wanaofika hapo
kila mara jijini Madrid wakiajribu kukutana naye na kusaka taarifa
mbalimbali
Ripoti iliyotolewa na jarida la El Mundo linasema kuwa hali ilikuwa
mbaya na ambayo haikuwa na faida kwa baadae na kibiashara kutokana na
suala hilo kuwa nje ya uwezo
Baadhi wa waandishi walifikia hatua ya kujifanya wateja ili tu wapate
taarifa za Rodriguez ambazo wangeweza kuziandika ama kuziripoti.
Baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili na mabosi wake,
binti huyo mwenye umri wa miaka 22 ilimbidi kuachia nafasi yake.
Na kazi ya Prada haikuwa ya kwanza kwenye suala la mitindo ambalo
Rodriguez amejikita ambayo kapoteza kwani kutokana na mahusiano yake na Cristiano Ronaldo ilibidi aache kazi kwenye kampuni ya Gucci.
Aliondolewa na uongozi wa Gucci mwisho wa mwezi November, huku mabosi
wakihofia kuwa wingi na uwepo wa waandishi kila mara ungeathiri
mahusiano yao na wadau wao na wahisani.
Tuesday, April 11, 2017
New
“Demu” Wa Ronaldo Aondolewa Kazini Kwa Sababu Ya Bwana Ake.
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment