FAHAMU RATIBA YA LIGI KUU WEEKEND HIII - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, April 11, 2017

FAHAMU RATIBA YA LIGI KUU WEEKEND HIII

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea Alhamisi Aprili 13, 2017 kwa timu ya Mbeya City kuikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Stand United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Toto Africans ya Mwanza itaialika Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya
Pwani kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani ilihali JKT Ruvu ikiwa kwenye Uwanja wake mpya wa nyumbani – Mkwakwani jijini Tanga itaialika Azam ya Dar es Salaam.

Jumapili Aprili 6, mwaka huu Mbao itacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Mwadui ikiwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mwadui  mkoani Shinyanga.

No comments:

Post a Comment