IKOSI cha Yanga SC kitaondoka Dar es Salaam Alhamisi wiki hii kwa ndege ya Shirika la Kenya kwenda Lusaka, Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki.
Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo katika mazungumzo na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba msafara huo utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi kadhaa ambao watatajwa baadaye.
Katika mchezo wa juzi, uliochezeshwa na maarefa kutoka Djibouti, Djamal Aden Abdi aliyeyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime, Yanga walitangulia kwa bao winga wake machachari, Simon Happygod Msuva dakika ya 39, kabla ya Zanaco kusawazisha dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame.
Yanga sasa watalazimika kwenda kushinda ugenini katika mchezo wa marudiano mwishoni mwa wiki ili kusonga mbele hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment