Itakuwa ni mara ya pili kukutana mwaka huu, kwani zilipambana kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar Januari.
Pia itakuwa ni mechi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, kwani zilikutana Oktoba Mosi mwaka jana kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza na kutoka sare ya bao 1-1.
Ni mechi itakayowafanya baadhi ya wachezaji waingie kwenye rekodi mbali mbali za pambano la watani wa jadi.
Wafuatao ni wachezaji ambao kama wakicheza au kufunga wataweka rekodi zao binafsi kwenye mechi hiyo.
Daniel Agyei-Simba
Daniel Agyei
Hapana shaka kuwa ndiye atakayekaa golini Februari 25. Ataweka rekodi ya kudaka mechi ya kwanza ya watani wa jadi kwenye mechi za Ligi Kuu.
Pia itakuwa ni mara ya pili kukaa golini dhidi ya Yanga, kwani ameshafanya hivyo mjini Zanzibar, Kombe la Mapinduzi.
Justine Zullu-Yanga
Justine Zullu ( Picha hisani )
Kama atacheza, itakuwa ni mechi ya kwanza ya watani wa jadi. Mchezaji huyo raia wa Zambia, alisajiliwa kipindi cha dirisha dogo katikati ya msimu huu.
Ibrahim Ajibu-Simba
Ibrahim Hajib
Akifunga goli, litakuwa ni bao lake kwa kwanza kwenye mechi ya Simba na Yanga. Hajawahi kufunga goli kwenye mechi ya watani wa jadi, tangu aanze kuichezea Simba msimu wa 2014/15.
Obrey Chirwa-Yanga
Itakuwa ni mechi yake ya kwanza kuichezea Yanga dhidi ya Simba. Hakucheza kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza. Akifunga bao litakuwa la kwanza kuifunga Simba.
Shiza Kichuya-Simba
Akifunga goli, litakuwa la pili kuifunga Yanga kwenye mechi mbili mfululizo. Ikumbukwe kuwa ndiye aliyefunga bao la kusawazisha kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu, Oktoba Mosi, dakika ya 87.
Pia itakuwa ni mechi ya pili kuichezea Simba dhidi ya Yanga.
Donald Ngoma-Yanga
Straika huyu wa Yanga, kama akifunga goli litakuwa ni la pili kuifunga timu hiyo, tangu alipojiunga na timu hiyo msimu wa 2015/16.
Ngoma aliifungia Yanga goli dhidi ya Simba Februari 20, 2016, alipoukuta mpira uliorudishwa kizembe na Hassan Kessy, Yanga ikishinda mabao 2-0.
Laudit Mavugo-Simba
Atakuwa akicheza mechi yake ya pili dhidi ya Yanga kwenye mechi za Ligi Kuu. Raia huyu wa Burundi, alicheza kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza, lakini alidhibitiwa vema na mabeki wa Yanga, na hakung’ara kabisa.
Akifunga litakuwa ni goli lake la kwanza kwenye mechi za mahasimu wa jadi.
Amissi Tambwe-Yanga
Akifanikiwa kufunga goli, litakuwa ni la nne mfululizo kuifunga Simba kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tambwe, aliyejiunga na Yanga akitokea Simba katikati ya msimu wa 2014/15, amefunga goli moja kwenye mechi tatu mfululizo za ligi ambazo timu yake ilicheza dhidi ya Simba.
Bao lake la kwanza lilikuwa ni Septemba 26, 2015, Simba ikilala kwa mabao 2-0 na mechi ya mzunguko wa pili Februari 20, 2016 akifunga, Yanga ikishinda tena mabao 2-0. Mechi zote ni za msimu wa 2015/16.
Oktoba Mosi, 2016, mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu, alifunga goli timu yake ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba.
Juma Luzio-Simba
Akifunga goli litakuwa ni la kwanza kwenye mechi ya watani wa jadi. Straika huyo wa Kibongo, zamani akiichezea Mtibwa Sugar, ndiyo kwanza amejiunga kwenye kipindi cha dirisha dogo msimu huu akitokea Zesco ya Zambia kwa mkopo.
Simon Msuva-Yanga
Hajaifunga Simba goli lolote lile kwa misimu mitatu sasa. Mara ya mwisho kufunga bao dhidi ya Simba ilikuwa ni Aprili 19, 2014,
Ligi Kuu msimu wa 2013/14.
Amecheza mechi sita za watani wa jadi bila kufunga goli, licha ya kwamba ni mmoja wa wafungaji viongozi kwenye timu ya Yanga.
Akifunga goli Jumamosi, litakuwa ni goli lake la pili kuifunga Simba tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2012 akitokea Moro United.
No comments:
Post a Comment