WALCOT APIGA BAO LA 100 ARSENAL - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, February 21, 2017

WALCOT APIGA BAO LA 100 ARSENAL

Mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Theo walcott, amefikisha mabao 100 ya kufunga
akiitumikia timu yake, baada ya kufunga bao katika mchezo wa Kombe la FA uliopigwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Sutton United uliomalizika kwa ushindi wa Arsenal wa mabao 2-0.

Kocha Arsene Wenger aliwachezesha wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza wakiwemo Walcott, Mohamed Elneny, Gabriel Paulista na Skhodran Mustafi huku Alexis Sanchez akiwekwa benchi.

Baada ya kuanza kwa kusuasua, washika bunduki walipata bao la kwanza dakika ya 27 kupitia kwa Lucas Perez aliyeambaa na mpira kutokea kushoto kabla ya kuachia shuti lililojaa kimiani.
Sutton, walitumia muda mwingi kuzuia kutokana na Arsenal kutawala pambano japokuwa walionesha uhai kila mara waliposhambulia kwa kushtukiza.
 Image result for WALCOT
Licha ya Arsenal kutawala pambano, bado walijikuta wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 tu.

Dakika kumi baada ya kipindi cha kuanza, Walcott aliipatia Arsenal bao la pili na kutimiza mabao 100 tangu ajiunge na kikosi cha Wenger.

Sutton walikaribia kupata bao dakika ya 65 kupitia kwa Rory Deacon ambaye shut lake kali liligonga mwamba wa juu

Arsenal waliendelea kutawala mchezo licha ya Wenger kuamua kuamua kuwapa nafasi Sancheza na Maitland-Niles katika robo saa ya mwisho.
Kwa matokeo hayo, Arsenal imefuzu kwa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA  ambapo wamepangwa kucheza dhidi ya Lincoln City.

No comments:

Post a Comment