Mwamuzi Mark Clattenburg ameamua kubadili uamuzi wake wa kuachana na Ligi Kuu Uingereza mara moja.
Awali Clattenburg alipanga kutochezesha
mechi zaidi Ligi Kuu Uingereza kufuatia kuingia mkataba mnono wa kuwa
mkuu wa kitengo cha waamuzi nchini Saudia Arabia.
Baada ya masahauriano baina yake na
viongozi wa kitengo cha waamuzi Uingereza, Clattenburg ataendelea
kuchezesha mechi za Ligi Kuu hadi mwisho wa msimu huu.
Ataanza majukumu yake nchini Saudia Arabia
baada ya kumalizika msimu. Tayari amerudi Uingereza na anatarajiwa
kuchezesha pambano kati ya West Borom na Bournemouth siku ya Jumamosi.
Hata hivyo anaweza asipangwe kuchezesha
mechi kubwa kama ile ya Arsena na Liverpool ambayo kwa kawaida huwa
anapewa kuchezesha kutokana na ubora wake.
No comments:
Post a Comment