Singida United imefikisha pointi 30 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka kundi C, na kufanya msimu ujao wakazi wa mkoa huo kushuhudia uhondo wa VPL uwanja wa Namfua.
Katika mchezo mwingine Panone wametoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora leo katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Kikosi cha Fred Felix Minziro kimefikisha pointi 30 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi, Alliance Schools 26, Rhino Rangers 25
Mpaka sasa timu mbili zimeshapanda kucheza Ligi Kuu msimu ujao, Lipuli kutoka kundi A na Singida United kutoka kundi C.
Timu moja inasuburiwa kutoka kundi B lenye upinzani kati ya Polisi Moro, Kinondoni Manispaa, Njombe Mji ikiwa imbakia michezo miwili kabla ya kumalizika kwa michezo ya kundi hilo.
No comments:
Post a Comment