APR wajiweka sawa kurudiana na Yanga, waibana Zanaco - ALEX MWENDATZ

Breaking

Saturday, February 11, 2017

APR wajiweka sawa kurudiana na Yanga, waibana Zanaco

Wawakilishi wa Rwanda katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, APR  ya Rwanda wameweza kuwabana wapinzani wao, Zanaco FC ya Zambia na kupata sare ya bila kufungana ugenini.

Katika pambano hilo lililopigwa leo, Zanaco walikaribia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Saith Sakala lakini mshambuliaji huyo alishindwa kulenga lango na kupoteza nafasi dakika ya 39.
APR walijibu mapigo dakika tatu baadaye kupitia kwa Patrick Sibomana kufuatia mpira wa kona lakini walinzi wa Zanaco walifanikiwa kuokoa hatari hio.

Dakika moja kabla ya mapumziko, alikuwa ni Sibomana tena aliyekaribia kupata bao pale shuti lake lililopotua katika nyavu ndogo kwa ahueni ya wenyeji wao.

Kwa matokeo hayo, APR ambao walitolewa na Yanga mwaka jana katika hatua ya raundi ya kwanza watahitaji ushindi wa aina yoyote kusonga mbele.

Pambano la marudiano litachezwa Jumamosi ijayo jijini Kigali, Rwanda katika uwanja wa Amahoro. Mshindi baina ya APR na Zanaco atakutana na mshindi baina ya wawakilishi wa Tanzania, Yanga na wawakilishi wa Comoro Ngaya ambao wanacheza mechi ya awali kesho.

No comments:

Post a Comment