Si mashabiki tu hata uongozi wa Simba ulikuwa na mashaka naye na ndio kisa cha kupewa mkataba mfupi wa miezi sita tu.
Kuchezea klabu kubwa za Afrika, TP Mazembe ma Esperance ya Tunisia kulitosha kudhihirisha kipaj chake lakini hofu na wasiwasi ulitokana kuwa alitokea Ligi ya Rwanda na si moja kwa moja kutoka klabu kubwa. Kutoka TP Mazembe hadi kuchezea Ligi ya Rwanda kulionekana kama ishara ya machweo ya soka lake.
Hakuwajaza mashabiki matarajio makubwa kiasi cha kutozungumziwa katika mechi yake ya kwanza jijini Dar iliyokuwa dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.
Hauonesha kasi ya kupanda na kushuka lakini kamwe hakupitwa na mshambuliaji yeyote. Alitimiza majukumu yake ya ulinzi bila mbwembwe.
Kadri siku zilivyosonga mbele ndivyo mashabiki walivyozidi kumuelewa. Injili yake ya kutumia uzoefu kuwazima washambuliaji wa Ligi Kuu iliwaingia wengi na hatimaye akaanza kuzungumziwa kama mmoja wa mhimili wa safu ya ulinzi ya Simba.
Mashaka ya kutomuamini yakageuka mashaka ya kukosa amani alipokosekana. Katika mechi dhidi ya ya Azam alilazimika kucheza kwa kudungwa sindano huku akiwa na kidonda kikubwa cha ‘shilingi’ licha ya kuwa msaidizi wake Hamad Juma alikuwa mzima kabisa.
Turejee kwenye pambano la jana ambapo ndani ya sekunde tatu mnamodakika ya 54 Bokungu alionesha ‘uzee’ na uzoefu wake.
Kwanza alionesha kuwa hana kasi pale alipozidiwa mbio na Obrey Chirwa baada ya makosa ya Said Ndemla na Abdi Banda ya kushindwa kucheza mpira wa juu.
Bokungu hawezi kukwepa lawama kwa kuonesha udhaifu katika kuondoa hatari. Si sawa kumbebesha mzigo wote dhambi Bokungu na kusahau makosa ya Banda na Ndemla na pia kasi na nguvu za Chirwa katika sekunde hizo mbili.
Kuteleza si kuanguka pamoja na kutenda kosa la kumruhusu Chirwa kumpita, Bokungu alitumia uzoefu wake kuepusha shari kamili na fedheha kwa Simba.
Kumbuka Chirwa alikuwa anaamba kuelekea ndani ya eneo la 18, Bokungu aliamua heri nusu shari ya kumchezea kumvuta na kumuangusha Chirwa kuliko kumruhusu aingie ndani ya 18 .
Akijua fika kuwa ni mtu wa mwisho alicheza ndivyo sivyo na kuzawadiwa kwa haki kabisa kadi nyekundu. Kinyume na hapo aidha angechelewa na kucheza rafu akiwa ndani ya 18 kama Lufunga alivyofanya au angemuacha Chirwa amsalimie Agyei. Vyovote vile ilikuwa ni hatari kwa Simba kupigwa bao la pili ambalo lingewamaliza kabisa Simba na kuzika matumaini ya kukomboa bao na hatimaye kushinda.
Kumbuka suala la walinzi wetu kuzubaa kufanya maamuzi na hatimaye kutenda madhambi ndani ya 18 ni janga la taifa katika soka letu. Timu zetu kuanzia vilabu hadi timu za Taifa zimekuwa zikiangushwa na makosa ya walinzi kuchelewa kusahisha makosa yao wakiwa nje ya 18.
Nyuso
za huzuni za mashabiki wa Simba wakati wakiwa nyuma kwa bao 1-0 na
mchezaji mmoja pungufu baada ya kadi nyekundu ya Bokungu.
Kwa dakika 54 alizodumu uwanjani, Bokungu alionesha uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi ya Yanga na hata katika tukio la kutolewa nje alituachia mafundisho kadhaa ya uzoefu na kutupa tofauti kubwa
No comments:
Post a Comment