P Mazembe, Mamelodi kuoneshana ubabe leo - ALEX MWENDATZ

Breaking

Saturday, February 18, 2017

P Mazembe, Mamelodi kuoneshana ubabe leo

Wababe hawa wanakutana baada ya msimu uliopita Mamelodi Sundowns kutwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe wakiibuka na ubingwa wa Kombe la Shirikisho
.
Hii ni mechi ya 25 ya kuwakutanisha Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho huku TP Mazembe ikiwa ni mechi yao ya nne wakati Mamelodi Sundowns wanacheza kwa mara ya kwanza.

Mazembe walioshinda taji hili mara tatu, mwaka 2010, 2011 na 2016 watakuwa chini ya kocha mpya, Thiery Froger aliyechukua mikoba ya kocha Hubert Velud japo makocha wasaidizi Pamphile Mihayo Kazembe na David Mwakasu wana uwezekano mkubwa wa kuongoza jahazi leo.
 Image result for mamelodi sundowns
Kocha wa Mamelodi Sundowns, Pitso Mosimane amekiri kuupa kipaumbele mchezo wa leo kuliko ule wa Ligi dhidi ya Chippa United uliomlizika kwa sare.
Mshambuliaji nyota wa Sundowns, Khama Billiat amesema mechi ni ya kipekee na kigezo halisi cha ukubwa wa klabu barani Afrika.

” Litakuta pambano kubwa. Hakuna pambano kubwa zaidi ya hili katika ngazi ya klabu. Mechi kama hizi ndio kipimo pekee cha ukubwa au ubora.” Amenukuliwa Billiat
Kwa upande wa TP Mazembe, kikosi chao kitawakosa nyota wao wanne, Rodger Assale, Jonathan Bolingi, Mervilleu Bope na Christian Luyindama waliouzwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment