NANI KUPISHA NAFASI ZA LIPULI, SINGIDA UNITED LIGI KUU MSIMU UJAO? - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, February 12, 2017

NANI KUPISHA NAFASI ZA LIPULI, SINGIDA UNITED LIGI KUU MSIMU UJAO?

Na Alex Mwenda
Ligi kuu bara inazidi kuyoyoma huku vilabu vya Simba na Yanga vikizidi kuchuana vikali katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu hivi sasa. Simba wameludi kileleni baada ya jana kushinda mabao 3-0 dhidi ya Tzs Prisons katika uwanja wa taifa na sasa wanashika usukani wakiwa na tofauti ya alama mbili na Yanga, ambao hii leo wanashuka dimbani kucheza na Ngaya club ya comoro mchezo wa awali ligi ya mabingwa.
 Image result for vodacom premier league
 Huku chini katika msimamo vita nayo ni kubwa sana Ruvu stars wana alama 16, Ndanda nao wako dhohofu bini hali, majimaji nao wanakabana koo na Toto kwa alama 21, pia Afrika lyon nao hawako katika nafasi nzuri.

Sasa timu mbili zimekwisha kukata tiketi ya kucheza ligi kuu msimu ujao ambazo ni Lipuli ya Iringa, pamoja na Singida united, bado hajafahamika ataepanda ligi katika kundi B ambako kuna timu za KMC, POLISI MORO, NJOMBE MJ na JKT MLALE ambao wote wana nafasi ya kupanda ligi.

 Nani atapanda katika kundi B na nani atashuka ligi kuu msimu huu? Wengi wanasemas Jkt ruvu ndo basi tena ila bado wanayo nafasi ya kujitetea zaidi ili wabaki ligi msimu ujao. Vita bado ni ngumu.

1 comment: