WENGER BADO KITI KITAMU ARSENAL - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, February 12, 2017

WENGER BADO KITI KITAMU ARSENAL

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewashukuru waandishi wa habari kwa kumtaka apumzike lakini amewaambia wazi, “wasahau”.

Wenger amesema hana mpango wa kuachia ngazi licha ya kuwepo kwa taarifa Arsenal ingependa kumchukua Diego Simeone kutoka Atletico Madrid ya Hispania kuchukua nafasi yake.


Mara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City yeye akiwa jukwaani, Wenger amesema, hana mpango wa kupumzika.

“Nashukuru sana kwa nia yenu njema ya kunitaka kupumzika. Lakini sihitaji kufanya hivyo kwa sasa,” alisema Wenger.

No comments:

Post a Comment