Na Alex Mwenda
Kocha wa Singida United Fred Felix Minziro amesema sapoti kubwa kutoka
kwa mashabiki wa Singida ndio sababu pekee ya timu yao kupanda daraja
na kurejea ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.
Kocha huyo wa zamani wa Yanga amesema, malengo waliyojiwekea
yametimia kwa kiasi kikubwa baada ya kufanikiwa kupanda kucheza VPL
msimu ujao.
“Ushirikiano wa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki
ambao wametupa sapoti kubwa kuhakikisha tunapata ushindi. Siri kubwa ya
ushindi wetu ni sapoti kubwa tuliyoipata kutoka kwa mashabiki wetu” –
Fred Felix Minziro.
“Malengo tuliyokuwa tumejipangia Singida United yametimia katika
kiwango kikubwa kwa maana kwamba tumeweza kuifunga timu ngumu kama
Alliance japo mechi ilikuwa ngumu.”
Mashabiki wengi waliingia uwanja wa Namfua mjini Singida kushuhudia
mchezo wa soka ligi daraja la kwanza kati ya Singida United dhidi ya
Alliance kutoka mkoani Mwanza mchezo ambao umeipa nafasi Singida United
kurejea ligi kuu Tanzania bara baada ya kusota kwa zaidi ya miaka 10.
Singida United ilipata ushindi wa magoli 2-0, mkongwe Nizar Khalfan
alianza kuifungia Singida bao la kuongoza dakika ya 14 baada ya mabeki
wa Alliance kuzembea kwa kudhani Nizar alikuwa ameotea.
Kipindi cha pili Singida United wakaandika bao la pili kwa mkwaju wa
penati uliopigwa Rashid Gumbo baada ya mchezaji wa Alliance kuunawa
mpira kwenye box.
Singida United sasa rasmi wamepanda daraja baada ya Rhino Rangers
ambao pia walikuwa na nafasi kulazimishwa sare huko mkoani Kilimanjaro
dhidi ya Panone na kuiacha Singida United ifikishe pointi 30 ambazo
haziwezi kufikiwa na timu yeyote ile kutoka kwenye kundi lao.
Sasa wakazi wa mkoa huo kuzishuhudia timu zote za ligi kuu katika uwanja wa Namfua
Sunday, February 12, 2017
New
MALENGO NA MIPANGO ILIVYOTIMIA KWA SINGIDA UNITED, KOCHA ATOA YA MOYONI
About SPORTS ROOM
SoraTemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of SoraTemplates is to provide the best quality blogger templates.
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment