Wakati Yanga wakiwa dakika 180 tu kuweka rekodi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya pili, Shirikisho la Soka Barani Afrika limeshapanga waamuzi wa pambano la awali kati ya wawakilishi hao wa Tanzania Bara dhidi ya Zanaco ya Zambia.
Mwamuzi wa Djibouti Djamal Aden Abdi ndiye atakayeamua dakika 90 za mchezo huo akisaidiwa na Hassan Egueh Yacin na Farhan Bogoreh Salime wote kutoka Djibouti.
Mwamuzi wa akiba ni Souleiman Ahmed Djamal kutoka Djibouti na kamisaa wa mechi kutoka Ethiopia, Luleseged Begashaw Asfaw
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa unatarajiwa kuchezwa Machi 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukitarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kwani licha ya kuwa Yanga haina historia ya kufanya vizuri inapokutana na vilabu vya Zambia, wengi wanaamini hii ni fursa adimu kufuzu hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment