ILE MILIONI 600 YA YANGA NI LINI? JIBU HILI HAPA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Saturday, May 12, 2018

ILE MILIONI 600 YA YANGA NI LINI? JIBU HILI HAPA

Unakumbuka baada ya Yanga kufanikiwa kuitoa Welayta Dicha ya Ethiopia kwenye mchezo wa mtoano wa Caf Confederation Cup kuingia makundi watu walisema Yanga wamepewa milioni 600?
Ni kweli ukishiriki Makundi ya kombe la shirikisho (Caf Confederatio Cup) na ukamaliza nafasi ya 3 au ya 4 kwanye kundi utapata zawadi ya USD 275,000 ila ukimaliza nafasi ya kwanza na ya pili wanafuzu robo fainali timu ambazo zimefungwa robo Fainali zitapata USD 350,000. timu zilifungwa nusu fainali zitapata USD 450,000 na Bingwa kupewa USD 1,250,000 na aliyefungwa fainali atapewa USD 625,000.
Hizo ndio Zawadi kwa Kombe la Shirikisho ila utaratibu wa kuzitoa huanza baada ya mechi za makundi kuisha kwa klabu ya Yanga mechi zake za kundi D zitaisha August 29 baadae September 02 kwenye draw ya robo fainali kutakuwa na kikao cha kamati tendaji ya CAF na kamati ya fedha kuangalia malipo ya timu baada kumaliza makundi.
Iwapo timu itakuwa inadaiwa fedha na CAF watakatwa kwenye fedha hizo hizo timu au mchezaji akiadhibiwa kwa kutozwa faini timu itakatwa kwenye fedha hiyo hiyo wanacalculate fedha unayodaiwa wanakata ndio unalipwa fedha hizo.
Pia kama klabu itashindwa kumaliza mechi za makundi itapigwa faini na kufungiwa kushiriki mashindano ya CAF na fedha hiyo hawatapewa hata kidogo na faini wanayolipa wanatoa wao tofauti na hiyo milioni 600.
Milioni 600 ya Yanga Sc ni September watu wanachangaya wengine wanasema fedha ilishaletwa na wengine wanalalamika Yanga wamepata milioni 600 za CAF harafu wachezaji wanashinikiza kulipwa madai yao ya mishahara ukweli ndio huo milioni 600 kuanza kutolewa mwezi wa tisa (September).
Kila kheri Yanga

No comments:

Post a Comment