SHIPOLOPOLO WATUA TANZANIA KUWAVAA TWIGA STARS JUMATANO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, April 2, 2018

SHIPOLOPOLO WATUA TANZANIA KUWAVAA TWIGA STARS JUMATANO


Kikosi cha wachezaji 30 wa timu ya soka ya Taifa ya wanawake ya Zambia(She-Polopolo) wamewasili nchini tayari kwa ajili ya mchezo wa awali dhidi ya Tanzania wa kuwania nafasi ya kucheza michuano ya Afrika mwaka huu.

Kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi siku ya Jumanne kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambao ndio utatumika kwenye mpambano huo.

Makipa: Catherine Musonda (Zesco United), Annie Namoonje (Ndeni), Bupe Mwanza(Buffalos), Rebecca Chola (Ndola School of Nursing).

Walinzi: Jacqueline Nkole(Indeni), Margaret Belemu (Red Arrows), Mercy Nthala (Green Buffalo), Lweendo Chisamu (Green Buffalos), Jane Chalwe(Zesco United), Marvis Kapando (Moba Queens), Mweemba Lushomo (Nkwazi), Aliness Kasoma (National Assembly).

Viungo: Mary Mwakapila (Green Buffaloes), Maylan Mulenga(Green Buffaloes), Hellen Chanda (Red Arrows), Rachael Lungu (Red Arrows), Prisca Chilufya (Red Arrows),Gloria Mwewa (Red Arrows), Rabecca Nyirenda (Red Arrows), Mary Mambwe(Nkwazi), Rhoda Chileshe (Zesco).

Washambuliaji: Misozi Zulu(Indeni), Esther Mushota (Moba Queens), Racheal Kunda Mwanje (Konkola Blades), Kunda Mwanje, Theresa Chewe (Ndeni), Ireene Zulu(Chiparamba), Agnes Musesa (Buffaloes), Havel Chitundu (Zesco), Christabel Phiri (National Assembly).

Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.
Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia na Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo wa Wanawake Afrika, ambazo zitafanyika nchini Ghana mwaka huu.

No comments:

Post a Comment