Mfahamu Paul Bukaba wa klabu ya Simba - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 11, 2018

Mfahamu Paul Bukaba wa klabu ya Simba

HUYU NDIYE PAUL BUKABA
Wengi walikuwa na hofu kuwa kukosekana kwa Erasto Nyoni, Kotei na Juuko kungeleta tatizo kwenye safu ya ulinzi ya Simba katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar jana.
Lakini mlinzi huyo ambaye amekuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, alithibitisha kuwa Simba imekamilika msimu huu.
Bukaba alionesha kiwango bora kabisa kwenye mchezo huo ambapo Simba iliibuka na ushindi wa goli 1-0.
Baaada ya mchezo Bukaba aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo kwa upande wa Simba Sc.
Beki huyo alishirikiana vyema na beki mwenzake Yusuph Mlipili kabla ya kuingia kwa Salim Mbonde na wote wakahakikisha Mtibwa Sugar hawafungi goli lolote.

No comments:

Post a Comment