Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce yuko tayari kumsaini mchezaji huyo wa Uingereza kwa uhamisho huru huku kandarasi ya Wilshere ikiisha mwisho wa msimu huu.. (Liverpool Echo)
Wenger pia yuko tayari kumpatia kandarasi mpya Santi Carzola 33, lakini hajui iwapo mchezaji huyo wa Uhispania atacheza tena.(telegraph)
Juventus iko tayari kumsaini mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania 25 Alvaro Morata lakini iwapo atakubali kupunguza mshahara wake.. (Sun)
Mmiliki mkuu wa klabu ya Bordeaux nchini Ufaransa amesema kuwa klabu hiyo huenda ikamuuza mshambuliaji wao raia wa Brazil Malcolm mwisho wa msimu huu. (Sudouest, via Goal.com)
RB Leipzig inataka kumsajili mshambuliaji aliye kwa mkopo Ademola Lookman, 20, kutoka Everton kwa mkataba wa kudumu (Daily Star)
Kungo wa kati wa Brazil Brazilian Andreas Pereira, 22, anasema kuwa lengo lake ni kurudi Manchester United na kuimarika baada ya kipindi chake cha mkopo katika klabu ya Valencia kukamilika. (South China Morning Post)
Brighton inataka kumsajili mshambuliaji wa Strasbourg na Cameroon Stephane Bahoken. (Express)
Wazo la kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba kurudi Juventus ni ‘ndoto’ kulingana na afisa mkuu wa klabu hiyo Giuseppe Marotta. (Mediaset, via Manchester Evening News)
Paris St-Germain wamewasiliana na ajenti Mino Raiola kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba. (ESPN)
United Itahitaji kulipwa £140m iwapo Pogba anataka kuondoka Old Trafford mwisho wa msimu huu miaka miwili baada ya kulipa dau lililovunja rekodi ya uhamisho la £89m ili kumsajili. (Mail)
Manchester City bao inamnyatia mshambuliaji wa Leicester na Algeria 27 Riyad Mahrez na inajiandaa kutoa kitita cha £65m mwisho wa msimu huu. (Sun)
Manchester United wanapigiwa debe kumsajili mshambuliaji wa Watford na raia wa Brazil 20 Richarlison mbele ya Bayern Munich na PSG. (Mail)
West Ham wanamnyatia kipa aliyepo kwa mkopo Joe Hart ,31, kutoka Manchester City kwa kanadarasi ya kudumu. (Mirror)
Usakaji wa saini ya mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu huu kutatokana na uwezekano wa iwapo raia wa Wales Gareth Bale ataondoka katika klabu hiyo. (Mail)
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatumai kiungo wa kati Jack Wilshere, 26, atatia saini kandarasi ya muda mrefu katika klabu hiyo. (Goal)
No comments:
Post a Comment