KIKOSI BORA CHA EPL MSIMU HUU - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, April 18, 2018

KIKOSI BORA CHA EPL MSIMU HUU

Manchester City wametawala kikosi bora cha mwaka cha Ligi kuu ya Soka ya Uingereza kwa kutoa wachezaji watano katika nyota 11 ambao wamewekwa wazi leo Jumatano.
Vijana wa Pep Guardiola wametwaa taji la EPL kwa mara ya tatu sasa na wachezaji wa kikosi hiko wamezawadiwa kuingia kwenye kikosi cha mwaka.
Beki wa kulia Kyle Walker, beki wa kati Nicolas Otamendi , Viungo David Silva na Kevin De Bruyne na Straika Sergio Aguero.
Kwa kushangaza ni mara ya kwanza kwa Sergio Aguero kuingia katika kikosi bora cha mwaka cha Ligi kuu ya Uingereza licha ya kuonyesha kiwango cha juu katika kila msimu tangu atue Uingereza.
Tottenham ndio timu nyingine ambayo imewakilishwa na wachezaji zaidi ya mmoja katika kikosi cha mwaka wakitoa wachezaji watatu, Beki Jan Vertonghen, kiungo Christian Eriksen na Straika Harry Kane.
Mchezaji pekee kutoka Manchester United ni David De Gea huku Chelsea wakiwakilishwa na Marcos Alonso.
Kinara wa upachikaji magoli katika ligi kuu ya Uingereza , Mohamed Salah ( Magoli 30 ) naye ni mchezaji pekee kutoka wana nusu fainali ya UEFA, Liverpool .
Nani ambaye amekosekana alistahili kuwepo ? au kikosi hiko ndio sahihi ?

No comments:

Post a Comment