Je Lwandamina atakuwepo kwenye mchezo wa Leo? Jibu la Meneja wa Timu hili hapa Yanga leo itakuwa mwenyeji wa timu ya Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam mchezo ambao unatarajiwa kuwa Mgumu kutokana na upinzani ambao umekuwepo kwa timu hizi zinapokutana kwenye michuano Mbalimbali. Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga George Lwandamina jana ametambulishwa rasmi na timu ya ZESCO kama ndiye kocha mkuu wa Timu ya ZESCO mara baada ya aliyekuwa kocha wa ZESCO kujiuzulu siku kadhaa zilizopita.
Lakini swali kubwa ni je Lwandamina atakuwepo kwenye mchezo wa Leo dhidi ya Singida United? Meneja wa Yanga Hafidh Saleh akizungumza na Kipindi cha Michezo cha Sports Extra cha Clouds Fm msomaji wa Kwata unit alisema Kocha atakuwepo kwenye mchezo wa Leo licha ya jana kutotokea kwenye mazoezi
No comments:
Post a Comment