Tetesi za soka barani Ulaya - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 21, 2018

Tetesi za soka barani Ulaya

DONDOO NA TETESI ZOTE ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO YA MARCH 21-2018
Chelsea inaongoza katika kumnyatia beki wa Ujingereza na Man United Luke Shaw, ambaye alikuwa shabiki mkubwa Chelsea akiwa utotoni mwake , iwapo ataamua kuondoka manchester United mwisho wa msimu huu. (Mail)

Maafisa wakuu katika klabu ya Manchester United wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu tabia ya Mourinho dhidi ya Shaw na hatua hiyo huenda ikaathiri thamnia ya uhamisho ya mchezaji huyo (Telegraph)

 Tottenham iko tayari kurudi Crystal Palace na dau la £40m kumsajili winga Wilfried Zaha, 25, lakini Crystal Palace inaamini kwamba mchezaji huyo ana thamnia ya juu zaidi..

(Mail) Ajenti wa mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, hajatoa hakikisho lolote kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo. (Il Bianconero, via Independent)

Tottenham imejiandaa kumpoteza beki wa ubelgiji Toby Alderweireld, 29, mwisho wa msimu huu lakini watahitaji kulipwa dau la Yuro 50m (£44m). (HLN - in Dutch) Liverpool imesema kuwa haitamuuza mshambuliaji wake Mohamed Salah, 25, mwisho wa msimu huu na kwamba mchezaji huyo wa Misri hana kandarasi itakayomruhusu kuondoka katika klabu hiyo wakati wowote. (ESPN)

Liverpool bado haijwasiliana na kipa wa Roma Alisson, 25, lakini raia huyo wa Brazil hayuko tayari kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Itali. (Sun)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 26, amepinga uvumi kwamba anatakakujiunga na PSG kwa kusema kwamba anahisi kuwa nyumbani Stamford Bridge.(Express)

 Mchezaji anayelengwa na klabu ya Manchester United Milan Skriniar, 23, anasema kuwa anafurahia kusalia Inter Milan .Ria huyo wa Slovakia pia ameivutia Barcelona . The Slovakian also interests Barcelona. (star)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anasema kuwa kujiamini ndio ufunguo wa ufanisi .Mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 amefunga mbao 21 katika mechi 13 tangu kuanza kwa msimu wa 2018.2018. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure hakushiriki katika mazoezi ya kwanza na timu ya taifa ya Ivory Coast siku ya Jumanne . (Fifciv.com) Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewapatia wachezaji wake ambao hawajiungi na timu zao za kimataifa likizo ya wiki moja huku akiwapeleka ,wasaidizi wake wa ukufunzi Tenerife.

 (Liverpool Echo) Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaipata mashakani na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kujihusisha na kampuni nyengine ya kucheza kamari.. (Mirror)

No comments:

Post a Comment