SINGIDA UNITED YAKANUSHA SUALA LA KUFUNGIWA KWA MCHEZAJI WAO - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 21, 2018

SINGIDA UNITED YAKANUSHA SUALA LA KUFUNGIWA KWA MCHEZAJI WAO

Image result for daniel lyanga


Mchezaji wetu Daniel Lyanga hajatungiwa miezi sita kucheza soka, Klabu yetu ya Singida United ilifuata taratibu zote za usajili wa mchezaji Daniel Reuben Lyanga, usajili ulishirikisha pande zote mbili kati ya Fanja Fc na Singida United ikiwemo kulipa fidia za gharama wa mkataba wake uliokuwa umebakia kule Fanja Fc.

Taratibu ambazo zilipekea klabu yetu kupata release letter ya mchezaji na kuendelea na hatua za kiusajili.
Kilichopo ni kwamba ITC ya Daniel Lyanga ilichelewa kuja kutokana na dirisha la usajili kufungwa, hivyo FIFA walituandikia barua kwamba ITC yake itakamilika hadi hapo dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa hapa Tanzania ( kunzia July/2018). Daniel Lyanga hajafungiwa na hivi tunategemea kumtumia kwenye michuano ambayo klabu yetu inakwenda kushiriki nje ya nchi.
Tunaomba vyombo vya habari kutumia taarifa rasmi kutoka vyanzo rasmi kwa maslahi ya mpira wa miguu hapa nchini.
Singida United milango yetu ipo wazi kutoa ushirikiano kwa jambo lolote ambalo chombo cha habari kinataka kujua, kufahamu au kushauri.


No comments:

Post a Comment