SAMWELI ETOO MCHAWI WA SOKA ANAETAKIWA KUKUMBUKWA KWA WAKATI WOTE - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, March 19, 2018

SAMWELI ETOO MCHAWI WA SOKA ANAETAKIWA KUKUMBUKWA KWA WAKATI WOTE

NA ALEX MWENDA
Siri ya kipaji ni mafanikio, na mafanikio huja kama unakitendea haki kipaji chako, na kipaji chako huonekana kama unapewa nafasi ya kuonesha kipaji chako…..mmmh lisikutishe hilo……..
Walimwengu humtambua kama shujaa wa soka wa bara la Afrika kwani uwezo wake ni wakumfananisha na JAY JAY OKOCHA, GEORGE WEAH, AL HAJI DIOF, mmh hata Mbwana Samatta huenda akawa ananusa harufu yake.
Huyo sio mwingine ni nyota wa Simba wa Afrika ambae alitamba na anaendelea kutamba katika ulimwengu huu wa mchezo huu wa mpira wa miguu.  Alizaliwa tarehe 10.03.1981 katika mji wa Douala maarufu sana nchini Cameroon.
Image result for SAMUEL ETOO
Kuna wakati mpaka mama wa mchezaji huyu aliuza kila kitu kumsafirisha mwanae akatafute maisha barani Ulaya. Kama sio huruma ya mama huyu tusingemfahamu SHUJAA WETU WA LEO NDANI YA KEYSPORTS……
Alianza kufanya mazoezi akiwa katika akademi ya Khadji sports, baada ya hapo alijiunga na timu ya vijana ya Real Madrid katika mwaka 1997, na alikuwa mchezaji mwenye kipaji cha pekee zaidi kutokana na kufanya mazoezi na timu ya pili ya Real Madrid.
 Alishindwa kucheza Segunda B kutokana nayeye kutoKUWA NA KIBALI cha kucheza soka barani Ulaya. Alitolewa kwa mkopo kuelekea klabu ya Leganes iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la pili mnamo mwaka 1997-1998 na alicheza michezo 30 na kufunga magoli manne pekee.
Samuel Etoo alilejea tena Real Madrid na kumalizia msimu wa mwaka 1998-1999. Katika mwezi januari 1999, alitolewa kwa mkopo kwenda Espanyol na hakuweza kucheza mchezo wowote klabuni hapo.
Msimu uliofuata katika dirisha la usajili majira ya joto alihamia ligi kuu laliga nchini Hispania  katika klabu ya Real mallorca kwa mkopo, na alifunga magoli 6 katika michezo 19. Mwishoni mwa msimu Samuel Etoo aliachana na Real Madrid na kusaini mkataba na Real mallorca kwa euro milioni 4.4 kama ada ya uhamisho.
Katika msimu wake wa kwanza alifunga magoli 11 katika ligi. Na kupewa sifa kede kede na aliekuwa raisi wa timu hiyo Mateo Alemany kuwa staili ya mchezaji huyo kuwa ya kipekee zaidi.
Aliisaidia Real mallorca kufika fainali ya Copa del rey dhidi ya Recreativo de Huelva katika mwaka 2003, mchezo ambao mallorca ilishinda mabao matatu kwa sifuri huku Etoo akifunga mabao mawili katia mchezo huo.
Kwa muda wote ambao Samuel Etoo aliichezea Mallorca aliweza kufunga mabao 54. mwaka 2004 katika kipindi cha majira ya baridi alisaini klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho wa euro 24 milioni baada ya makubaliano yaliyofanyika na timu za  Real Madrid na mallorca, huku kipengele cha Madrid kikiwekwa kuwa wakati wowote wakihitaji kumnunua waweze kamnunua.
Etoo alianza kuichezea Barcelona katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Racing Santanda tarehe 29.08.2004, baada ya Barcelona kushinda laliga msimu wa mwaka 2004-2005. Akiwa ametwaa ubingwa na wababe hao wa camp nou Etoo aliwaudhi mashabiki wa Real Madrid baada ya kuposti Madrid, bastards, salute tha champions, kwa tafasisi ni kwamba aliwaambia Madrid kuwa washamba na wanatakiwa kuheshimu mabwingwa.
Chama cha sheria na hadhi na wachezaji nchini Uhispania The Royal Spanish Football Federation kilimtoza euro 12,000 kwa maneno yake na kuamriwa kuomba radhi kwa mashabiki kutokana na matamshi aliyoyatoa. Kauli yake ilionekana kukerwa zaidi na maofisa wa Real Madrid ambao walimkuza walimpokea akitokea barani Afrika nma kumkuza kisoka.
Alisaini mkataba mpya na Fc Barcelona mnamo mwezi june 2005. Baada ya kukosa ufungaji bora almaarufu PICHICHI TROPHY ambayo inatolewa na Laliga, Etoo alizidiwa na  mshambuliaji wa Valencia David Villa katika tuzo ambayo ilitolewa katika mchezo wa may 20, 2006. Na aliiwezesha Barcelona kufunga mabao matano katika msimu wa mwaka 200-2006 michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Eto'o  alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Uefa katika nchi ambazo ni za ushindani barani Ulaya..
Alishinda pia tuzo ya mchezaji bora wa Afrika katika msimu….Na alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora na hakufanikiwa kushinda tuzo hiyo ambayo historia bado imeshikiliwa na muafrika George Weah kutoka Liberia.
Huo ndio ulikuwa mwanzo mzuri  wa safari ya Samueli Etoo.

TUZO BINAFSI
·        Young African Player of the Year: 2000[108]
·         
·        African Player of the Year: 2003, 2004, 2005, 2010[109]
·         
·        ESM Team of the Year: 2004–05, 2005–06, 2008–09, 2010–11[110]
·         
·        FIFA World Player of the Year Bronze Award: 2005[111]
·         
·        FIFPro World XI: 2005, 2006[112][113]
·         
·        UEFA Team of the Year: 2005, 2006[107]
·         
·        CAF Team of the Year: 2005, 2006, 2008, 2009, 2010, 2011
·         
·        Pichichi Trophy2005–06[114]
·         
·        UEFA Champions League top assist provider: 2005–06[115]
·         
·         
·        UEFA Club Forward of the Year: 2006[107]
·         
·         
·        Coppa Italia top goalscorer: 2010–11[119]
·         
·        Russian Premier League MVP Award: 2012–13[56]
·         
·        Golden Foot: 2015[120]
·         
REKODI ALIZOWEKA
·         

ETOO ana ndugu zake wawili ambao ni kaka zake David na Etienne ambao wote ni wachezaji pia wa mpira wa miguu.
Etoo ana watoto wane Maelle, Etienne, Siena na Lynn. Alioa mke  mnamo 6.julai.2007..Georgette ni mama wa watoto Siena na Lynn ambao wote anaishi nao Paris nchini Ufaransa. Kwa hiyo wewe mdada ambaye ulidhani Etoo hajaoa na kama una nafasi basi amejituliza kwa bibie Georgette….

No comments:

Post a Comment