Makamu wa raisi wa TFF akwama kuwasilisha rufaa yake - ALEX MWENDATZ

Breaking

Sunday, March 18, 2018

Makamu wa raisi wa TFF akwama kuwasilisha rufaa yake



Akizungumza  wakati akiwa kwenye mchakato huo, Wambura amesema kilichomkwamisha ni kukosa mtu wa kuipokea licha kufika ofisini hapo mara tatu.

Uamuzi huo wa Wambura umekuja Ikiwa ni takribani siku tatu tangu afungiwe kujihusisha na mambo yote yahusuyo soka, kutokana na makosa ya kimaadili, na hivyo anapinga adhabu iliyotolewa na kamati ya maadili ya TFF.

Naye wakili wa Wambura, Emmanuel Muganyizi, amesema lengo la mteja wake ni kuwasilisha barua hiyo ndani ya siku kwa mujibu wa kanuni, hivyo uamuzi walioufanya ni kwenda posta na kuituma barua hiyo kwa njia ya posta,

No comments:

Post a Comment