Wazee wa zamani walituachia misemo mingi yenye
maana kwa ajili ya kuiasa jamii ili iwe katika mwenendo ambao ni mzuri zaidi.
Lakini kizazi cha siku hizi ni ngumu kuamini misemo ya wazee wa kale kama
chelewa chelewa utamkuta mwana si wako tena, ngoja ngoja yaumiza matumbo, na
hata ule wa mficha maradhi kifo kitamuumbua.
Bado mnaficha
maradhi yenu ndani ya klabu ya MAJIMAJI msubili kifo kije kuwaumbua na
watu wapate nafasi ya kuzungumza, kwani asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
Kila shabiki na mnazi wa wanalizombe ukimhoji
majibu atakayokupa juu ya MAJIMAJI ni tayari hana matumaini ya kuiona timu hii
kwa msimu ujao
Mnawaludisha vipi mashabiki wa aina hii ambao
tayari kwao mioyo yao imekufa, na matumaini hawana tena juu ya klabu yao???
Mwarobaini mnao nyie viongozi lakini lazima
mkubali kuwa makocha wa timu wameishiwa mbinu za kubuni, leo hi timu imecheza
michezo 22 imekusanya alama 16 bado mnaendelea kuwakumbatia watu kama hawa
mkiwa bado mna matumaini ya kuwa watawapa alama 15 katika michezo iliyosalia
hakika hii ni ndoto ya Bunuwasi.
Kama timu imeshindwa kupata ushindi wowote nje ya
uwanja wa Majimaji mnatarajia miujiza ipi timu ipate matokeo nje ya majimaji
hivi sasa??
Wakati wote timu imekuwa ikicheza vizuri sana
lakini tatizo lipo kwenye benchi la ufundi, viongozi hamuwaoni hao na bado
mnawakumbatia tuu, kumbukeni kuwa Nungunungu hakumbatiwi, au mnapenda kuona
timu ikishuka daraja???
Niwakumbushe msimu wa 2014\2015 Tz prisonsi
ilikuwa dhohofu bini hari ikiwa chini ya kocha Jumanne chale waliketi chini
bila aibu walimtimua kocha wao na kumpa mikoba Abduri Mingange, Prisons ikabaki
ligi kuu, na msimu uliofuata walimtimua, lakini jee kama wangeendelea kuwa nae
leo hii wangekuwepo wapi????
Msimu uliopita
Ndanda fc walikuwa katika hali mbaya sana hali iliyoperekea wachezaji
kutoroka kambini lakini walikaa chini kwa kushirikiana na aliekuwa mkuu wa mkoa
wa Mtwara bi Halima Dendego na kumtimua kocha wao na kumpa mikoba Abduri
Mingange ambae aliinusuru timu kushuka daraja na baada ya mipango kukamilika
walimtimua Mingange.
Lazima tuukubali ukweli kuwa timu hii ya Majimaji
tangu ipande daraja msimu wa 2015/2016 haijawahi kuwa na kocha bora kama Karl
Ongala moja kati ya wakufunzi waliojijengea heshima kubwa sana katika soka la
Tanzania.
Mnashindwaje kutenga milioni kadhaa tena mpo na
mtu wa michezo ambae anawasaidia mbunge Damas Ndumbaro ambae ni msikivu sana
hasa katika yale yote yaliyo mema, leo hii bado mnaamini kuwa benchi lenu la
ufundi litawakomboa nawaambieni msaahau msipofanya mabadiriko.
Ule msemo usemao mkaidi hafaidi hadi siku ya iddi
ulikuwa na maana kubwa sana tunaamini kuna makanjanja katika timu ya Majimaji
ambao wao utawaona katika zile siku za mafungu na migao ya mapato ya mlangoni
hata malupulupu mengineyo, sasa mnashindwa kujiongeza, makanjanja wenzenu huwa
wanapigania timu ziendelee kuwepo katika ligi ili matumbo yao yapate unafuu,
lakini kwenu mnawaza kurubuni kwa muda mfupi.
Hakuna soka wala vilabu visivyo na makanjanja
ndani yake hata Simba, Yanga, Lipuli fc, Ndanda, Mwadui wajanja wajanja wapo
lakini wana wao wana muono wa mbele hasa katika kuipigania timu kwa namna
yeyote ile.
Mnakumbuka Njombe mji baada ya kupanda ligi
walikuwa chini ya Hassan Banyai wakamtimua baada ya kuona timu inapata matokeo
mabaya walifanya maamuzi, na kuwaachia Mlage wa kabange na Ally Bushiri, kwenu
mbona bado hamna maamuzi?
Tatizo la kufanya kazi kimazoea na kishikaji ndo
ambako kunaaribu taratibu za timu, lazima mtambue kuwa heshima ya klabu ni
matokeo leo hii mnajipa kazi kubwa sana kwenda kuheshimika kanda ya ziwa
kutokana na matokeo yenu.
Tujitafakari huko tunakoelekea mnadhani ni sahihi
au tupambane hapa tulipo, tuliwataka muitishe mkutano hamkufanya hivyo, ina
maana hamkuheshimu mchango na mawazo yetu, sasa tunawataka mfanye mabadiriko
katika benchi lenu la ufundi na msipofanya hivyo msitarajie miujiza yoyote ile.
Wanaruvuma tutawalamu sana katika hilo na hata
ikitokea mmeishusha daraja timu msione haya kujivua madaraka kwani muungwana
huchutama anapokosea.
Niwakumbushe mlibugi katika mkataba na TING,
mkala mwereka kwenye mkataba feki na SOKABET yote athari zake mmeziona, sasa na
katika hili mkibugi basi kwa herini, na mtambue mnakoenda ni kugumu zaidi kwani
yahitaji wazalendo haswa kusukuma gurudumu hili...
Msipo yafanyia kazi haya tukutane ligi daraja la
kwanza msimu ujao. Haya yote ni mema tuu kwa faida ya Wanaruvuma wote.
No comments:
Post a Comment