MAJIMAJI KUPIMANA NGUVU DHIDI YA MBEYA CITY - ALEX MWENDATZ

Breaking

Friday, March 30, 2018

MAJIMAJI KUPIMANA NGUVU DHIDI YA MBEYA CITY

Na Alex Mwenda-Songea
Klabu ya wanalizombe wa Majimaji ya mjini Songea inatarajia kushika dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya city mchezo utakaofanyika katika uwanja wa ccm wilaya Mbinga.
Mchezo huo unatarajia kuanza muda wa saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika mashariki na huenda ukatangazwa moja kwa moja na kituo cha redio mkoani Ruvuma KEYFM 90.5

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili hususani Majimaji ambao wapo katika janga la kushuka daraja msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara. Akizungumza na Alex MwendaTZ mjumbe wa kamati ya utendaji ya majimaji Salum Masamaki amedai maandalizi yamekwisha kufanyika na wapo tayari kwa ajili ya mechi.
"Maandalizi yamekamilika ndugu mwandishi na mechi hiyo kwetu ni kipimo tosha kujiandaa na mechi zetu za kanda ya ziwa' amesema Masamaki.

Mara baada ya mechi hii klabu ya Majimaji itasafiri kuelekea Shinyanga kukipiga dhidi ya Mwadui Fc April 7 mwaka huu.
Image result for MAJIMAJI FC

No comments:

Post a Comment