Kocha Njombe Mji Aanika Mbinu Za Kuimaliza Simba - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 28, 2018

Kocha Njombe Mji Aanika Mbinu Za Kuimaliza Simba


. Kocha Mkuu wa Njombe Mji, Ally Bushir amesikia tambo pamoja na majigambo wanayotoa wapinzani wao Simba wanaotarajia kukutana nao April 3 mwaka huu na kutamka kuwa wasiwachukulie poa kwani wamedhamiria kushinda mechi hiyo. 


Kocha Bushiri alisema kama Simba inauchukulia poa mchezo huo na kujiamini kwamba ni lazima waondoke na pointi tatu mbele yao imekula kwao. 


Alisema katika mchezo huo Njombe Mji inahitaji ushindi mnono ili kurudisha hali ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kimsimamo na kuepukana na janga la kushuka daraja. 


‘’Tuna mechi nane mkononi ambazo tukizitumia vizuri hususani mechi za nyumbani tutafanikisha lengo letu la kukusanya pointi kadhaa na kubaki kwenye Ligi Kuu msimu ujao,’’alisema Bushiri. 

Bushiri alisema kuanza vibaya kwa msimu wake wa kwanza siyo kwamba watamaliza vibaya isipokuwa kwa mzunguko huo timu ilikuwa bado haijatengamaa na ndiyo chanzo cha timu kutopata matokeo uwanjani. 


Alisema kwa sasa anaona kikosi chake kipo katika ‘motisha’ nzuri na anafurahi kuona wachezaji wanaonekana kuishika mifumo ya kuhakikisha wanapata ushindi kwa kila mechi iliyo mbele yao. 

No comments:

Post a Comment