JONAS MKUDE AKUMBANA NA MAJERAHA - ALEX MWENDATZ

Breaking

Monday, March 26, 2018

JONAS MKUDE AKUMBANA NA MAJERAHA

Image result for MKUDE
KIUNGO mahiri wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude leo alilazimika kubebwa baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kulia katika mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam.

Mkude aligongana na kiungo mwenzake, Muzamil Yassin wakati wa kugombea mpira na kuanguka chini huku akiugulia maumivu, kabla ya Daktari wa timu, Yassin Gembe kuingia uwanjani kumpatia huduma ya kwanza.

Lakini huduma hiyo haikumsaidia Mkude, kwani hakuweza hata kuukanyagia mguu ulioumia kiasi cha kubebwa kupelekwa kwenye chumba cha kuvalia nguo, kabla ya kurudishwa nyumbani kwa gari.
Dk. Gembe amesemakwamba atalazimika kusubiri hadi kesho ili kumfanyia vipimo Mkude ili kujua uzito wa maumivu yake.
J
VIDEO: JONAS MKUDE AKITIBIWA BAADA YA KUUMIA LEO

Wakati akiumia, habari njema ni kwamba majeruhi wa muda mrefu Simba SC, beki mzawa Salim Mbonde na kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima leo wamefanya mazoezi kikamilfu kuelekea mechi na Njombe Mji FC Aprili 3.
Simba SC watakuwa wageni wa Njombe Mji FC Aprili 3, mwaka huu Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuelekea mechi hiyo Mbonde na Niyonzima wameleta tumaini jipya kikosini.

Niyonzima yuko mazoezini kwa siku ya tatu leo Simba SC baada ya kurejea kufanyiwa upasuaji nchini India, wakati Mbonde ndiyo ameanza rasmi mazoezi leo.
Simba ilitoa sare ya 0-0 na Al Masry Machi 17 na kutolewa kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 Machi 7, mwaka huu kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika.

Na baada ya kutolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) Novemba mwaka jana wakifungwa na Green Warriors ya Mwenge kwa penalti baada ya sare ya 1-1, Simba SC wana nafasi moja tu kucheza michuano ya Afrika mwakani, ambayo ni kupitia Ligi Kuu ambako bingwa wake hucheza Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Na bahati nzuri kwao, Simba SC ndiyo wanaoongoza Ligi Kuu kwa wastani wao mzuri wa mabao baada ya kulingana kwa pointi na mabingwa watetezi, Yanga SC 46 kila timu, ingawa pia Wekundu wa Msimbazi wana mechi moja mkononi.   
Wakati huo huo: Kocha Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre aliyekuwa nyumbani kwao kwa mapumziko, amerejea jana na leo alikuwepo mazoezini Uwanja wa Boko Veterani kuiandaa timu kwa mchezo dhidi ya Njombe Mji FC Aprili 3.

No comments:

Post a Comment