James Harden atakata NBA nchini Marekani - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, March 21, 2018

James Harden atakata NBA nchini Marekani

Image result for James Harden
Wimbi la ushindi la michezo 13 mfululizo la Trail Blazers lilizimwa alfajiri ya leo baada ya James Harden kufunga vikapu 42 wakati Houston Rockets wakiichapa Blazers kwa vikapu 115 kwa 111.
Ukiacha Harden mwingine alikuwa ni Chris Paul ambaye katika ushindi huo aliongeza vikapu 22 na kuwafanya Houston kushinda michezo sita mfululizo huku huu ukiwa ushindi wao wa 23 katika michezo 24 iliyopita.
Kabla ya mchezo huu Blazers walikuwa wameshinda michezo 9 mfululizo katika dimba la Moda Center lakini pia kipigo hiki hakikumzuia nyota wao Al Farouq kushine katika mechi hii.
Katika mchezo mwingine alfajiri ya leo Marcus Morris alifunga vikapu 21 wakati Celtic wakiwabamiza wageni wao OKC Thunder kwa vikapu 
Farouq aliweka vikapu 22 katika mchezo huo ambao pia ulikuwa mgumu kwa Harden kutokana na kuzomewa kila mara alipokuwa akigusa mpira. Rockets watacheza dhidi ya Detroit huku Trail Blazers watacheza dhidi ya Boston Celtics.

No comments:

Post a Comment