KHAMIS MCHA VIALI ATUA KWA WAFUNGA BUTI WA PWANI - ALEX MWENDATZ

Breaking

Wednesday, August 2, 2017

KHAMIS MCHA VIALI ATUA KWA WAFUNGA BUTI WA PWANI

Lufunga akimchunga Khamis Mcha wa Azam katika pambano la Ligi Kuu
Siku nne kabla ya dirisha la usajili Ligi Kuu Tanzania Bara kufungwa, timu mbalimbali ziko katika hatua ya mwisho ya kukamilisha vikosi vyao.
Mojawapo ya timu zilizo katika mchakamchaka wa kujipanga kwa ajili ya msimu mpya ni  Ruvu shooting iliyokatika hayua za mwisho za kumnasa mshambuliaji wa zamani wa Azam, Khamis Mcha.
Mcha anajiungana kllabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kuachwa na Azam mwishoni mwa msimu uliopita.
Kukamilisha kwa uhamisho wake kutaongeza ukali wa safu ya ushambuliaji ya Ruvu Shooting iliyokuwa ikimtegemea zaidi mfungaji bora mwenza wa Ligi Kuu msimu uliopita, Abdulrahman Mussa aliyetupia mabao 14 sawa na Simon Msuva wa Yanga

No comments:

Post a Comment