Mshambuliaji wa zamani wa vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga Emmanuel Okwi ameendelea kuonesha kuwa anarudi kwenye kiwango chake cha zamani baada ya kufunga mabao matatu jana katika mchezo wa Ligi Kuu Uganda dhidi ya Onduparaka.
Okwi aliisaidia SC Villa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 uliowapeleka kileleni mwa msimamo licha ya kuwa alianza pambano hilo vibaya baada ya kukosa penati
.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda amefanikiwa kuifungia SC Villa mabao 6 katika michezo mitano aliyocheza tangu ajiunge nayo kwa mara ya tatu.
Villa ilimsajili Okwi kwa mkataba wa muda mfupi wa miezi sita baada ya kuwa ameamua kuvunja mkataba na klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark.
No comments:
Post a Comment