Rais wa zamani wa Chama cha Soka Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya ambaye pia aliwahi kuwa nahodha na mshambuliaji wa timu ya Zambia ‘Chipolopolo’ amejitoa katika mbio za kuwania nafasi ya uwakilishi wa CAF kwenye Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Bwalya (53) alikua anawania nafasi hiyo ya uwakilishi kwa kundi la nchi zinaongea lugha ya kiingereza Afrika (Anglofone) sambamba na Leodagr Tenga (Tanzania) na Kwesi Nyantakyi (Ghana).
Kufuatia kujitoa kwa Bwalya katika kinyanganyiro hicho, nafasi ya Rais wa zamani TFF na CECAFA, Leodgar Tenga kuwakilisha FIFA kwa nchi zinaongea kiingereza Afrika iko mikononi mwa wapiga kura.
Katika taarifa yake kiongozi huyo wa zamani wa Zambia amesema, ameamua kuchukua uamuzi huo wa kujitoa kugombea kwa faida ya umoja wa mpira duniani, huku akiwatakia kila la kheri wagombea wawili waliobakia.
Uchaguzi wa viongozi na wawakilishi mbalimbali wa CAF unatarajiwa kufanyika Machi 16, Addis Ababa nchini Ethiopia wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment