Himid Mao aweka rekodi Taifa Stars - ALEX MWENDATZ

Breaking

Tuesday, March 28, 2017

Himid Mao aweka rekodi Taifa Stars

Kiungo mkabaji wa Taifa Stars, Himid Mao ameweka rekodi ya kuichezea Taifa Stars mechi mfululizo tangu mwaka 2015.
Image result

Himid ambaye ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars na pia akikabidhiwa makukumu ya kuiongoza Taifa Strs katika mechi za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani amecheza mechi 11 mfululizo. Ni mchezaji pekee aliyecheza mechi zote za Taifa Stars tangu Septemba mwaka 2015.
Awali hakuwa akiitwa na kocha Mart Nooij lakini mara tu Boniface Mkwasa alipochukua usukani alimjumuisha katika kikosi na kumuanzisha katika pambano dhidi ya Nigeria lililopigwa mwaka Septemba 5, 2015 jijini Dar.
Kabla ya pambano baadhi ya wachambuzi na mashabiki waliguna kwa uamuzi wa Mkwasa kumuanzisha, hata hivyo haikumchukua Himid dakika nyingi tangu mpira uanze kutoa jibu sahihi kwa nini alistahili kuwa chaguo la kwanza.
Sifa yake ya kukaba kwa mabavu na juhudi kubwa ilimzima kabisa kama sio kumstaafisha kiungo Lukman Haruna wa Nigeria.
Kocha Sunday Oliseh alilazimika kumpumzisha Haruna dakika ya 36 tu ya kipindi cha kwanza baada ya kufunikwa kabisa na Himid kiasi cha Nigeria kutepeta katikati. Huo ndio ulikuwa mwisho wa Haruna kuitwa timu ya taifa ya Nigeria akiwa na umri mdogo wa miaka 26 kwa sasa.

No comments:

Post a Comment