Wauzaji wa tiketi hizo, kampuni ya Selcom tayari wameanza kuwatangazia mashabiki kununua tiketi kwa njia ya kadi za kampuni hio.
Ikumbukwe kuwa katika pambano la kwanza la watani msimu huu mashabiki walipata usumbufu mkubwa wa kununua tiketi kutokana na wengi kununua siku ya mwisho jambo lililopelekea mfumo wa kielektroniki kuzidiwa.
Pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kutokana na timu hizo mbilii kuwa katika vita kali ya kuwania ubingwa na pia kuchagizwa na matokeo ya Oktoba Mosi pale Amissi Tambwe alipofunga bao la utata kabla ya Shiza Kichuya kuisawazishia Simba kwa bao matata, litapigwa tarehe 25 Februari katika dimba la uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment